Thursday, August 16, 2012

ZAMARADI, RAY KIMENUKA.

Mtangazaji wa Kipindi cha ‘Take One’ cha Clouds Tv ya jijini Dar, Zamaradi Mketema na staa wa filamu za Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ kimenuka.
Chanzo kinasema kiini cha tifu lao ni kufuatia mtangazaji huyo kurusha kipindi akimuhoji mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ney wa Mitego akisema ‘ukitaka mwanamke malaya nenda Bongo Movie’. Baada ya kurusha kipindi hicho, inasemekana Ray alikereka na kuwataka wasanii wa Bongo Movie kutofanya kipindi na Zamaradi kwa madai aliwadhalilisha.

Zamaradi alipotafutwa kwa simu alikiri kusikia taarifa za Ray, akasema haoni kibaya alichokifanya kwenye kipindi hicho na hakuwa na nia ya kumdhalilisha mtu ila Ray amekuwa akimtafuta mara kwa mara.
“Mimi sijui Ray ananitafutia nini? Najua yeye ndiyo chanzo cha mambo yote, mbona mimi sina tatizo naye?” alihoji Zamaradi.
Ray aliposakwa na kupatikana alikiri kutoa matamshi hayo, lakini akasema hajamlazimisha msanii asihojiwe na Zamaradi, ila alishauri, atakayeona anapenda kuhojiwa ruksa.

No comments: