Tetesi za J'mosi magazeti ya Ulaya


LUIS NANI KUONDOKA MAN UNITED

Zenit St Petersburg sasa inamtaka winga wa Manchester United, Nani, mwenye umri wa miaka 25.
West Ham iko tayari kuzipiku Liverpool na Arsenal katika usajili wa mshambuliaji wa Fulham, Clint Dempsey, mwenye umri wa miaka 29.
Wakati huo huo, klabu hiyo ya Craven Cottage imekataa dau dogo la Manchester United kumtaka kiungo Moussa Dembele, 25.
Fulham midfielder Moussa Dembele
Moussa Dembele alijiunga na Fulham mwaka 2010
Beki wa Toulouse, Cheikh M'Bengue, mwenye umri wa miaka 24, amesema anatakiwa na Arsenal.
Stoke imeungana na Everton katika kuwania saini ya kiungo wa Liverpool, Charlie Adam, mwenye umri wa miaka 26.
Everton itamtoa kwa mkopo kiungo Ross Barkley, mwenye umri wa miaka 18, kwenda klabu ya Daraja la Kwanza, Sheffield Wednesday ambako wanaamini atapata uzoefu wa haraka wa kucheza katika kikosi cha kwanza.
Blackburn imeongeza ofa yake kwa ajili ya mshambuliaji wa Huddersfield, Jordan Rhodes, mwenye umri wa miaka 22.
Mshambuliaji Kevin Mirallas, mwenye umri wa miaka 24, atafanyiwa vipimo vya afya Everton mwishoni mwa wiki hii, kabla ya kukamilisha uhamisho wa pauni Milioni 5.3, akitokea Olympiacos.

OSCAR ASEMA HANA JAKAMOYO

Chelsea and Brazil midfielder Oscar
Oscar amewasili Chelsea akitokea Internacional
Mchezaji mpya wa Chelsea, Oscar amesema kwamba hasikii jakamoyo kabisa Stamford Bridge - kwa sababu tayari amefanikiwa kupata jezi namba 10 ya Brazil.
Sir Alex Ferguson amesema kwamba amekuwa mkali mno kwa wachezaji wake wa Manchester United wanaotumia Twitter, baada ya Rio Ferdinand kupigwa faini ya pauni 45,000 na FA.
Kiungo mstaafu wa Bolton, Fabrice Muamba atafanikiwa tu katika maisha yake kwa uamuzi wowote atakaochukua- kwa mujibu wa Nahodha, Kevin Davies.
Kipa wa Celtic, Fraser Forster amedhamiria kupambana kupata nafasi katika kikosi cha England kwa kufanya vitu adimu katika Ligi ya Mabingwa.