Tetesi za J'tano magazeti ya Ulaya


MAN UNITED WAIPIGA BAO NJE YA UWANJA MANCHESTER CITY

Kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amewapiku jirani zake, Man City katika kuwania saini ya mshambuliaji wa Chile, Angelo Henriquez, mwenye umri wa miaka 18.
Hulk
Mshambuliaji Mbrazil, Hulk anaweza kutua England
Arsenal inajipanga kumruhusu Robin van Persie, mwenye umri wa miaka 29, kujiunga na Manchester United kwa dau la pauni Milioni 22.
Lakini taarida nyingine zinasema kwamba Arsenal wanataka angalau pauni Milioni 25 kutoka Manchester United kwa ajili ya Van Persie.
Chelsea na Manchester City ziko mkao wa kula, kufuatia mshambuliaji wa Porto, Hulk, mwenye umri wa miaka 26, kusema yuko tayari kuihama klabu hiyo ya Ureno.
Manchester City inafikiria kuongeza vipaji zaidi vya Kiingereza kwenye kikosi chake, baada ya kumsajili Jack Rodwell na Scott Sinclair, Jack Butland na Nathan Redmond wakiwa wanatajwa kufuatiliwa na mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England.
Tottenham na Arsenal zitatakiwa kulipa pauni Milioni 28 kumsajili nyota wa kimataifa wa Hispania, Fernando Llorente, kwa mujibu wa rais wa klabu yake, Athletic Bilbao, Josu Urrutia.
Liverpool imemtuma Mkurugenzi wake Mtendaji, Ian Ayre kwenda Hispania kushughulikia usajili wa winga wa Barcelona, Cristian Tello, mwenye umri wa miaka 21, na kiungo wa Real Madrid, Nuri Sahin, mwenye umri wa miaka 23.
Andy Carroll
Mshambuliaji wa Liverpool, Carroll anaweza kutua West Ham
Everton inataka kutumia sehemu ya fedha ilizopata kutokana na mauzo ya Jack Rodwell, mwenye umri wa miaka 21, kwenda Manchester City kwa kumsajili Kevin Mirallas, mwenye umri wa miaka 24, kutoka Olympiacos kwa dau la pauni Milioni 6.
Habari kamili: The Times  (subscription required)
Vurnon Anita, mwenye umri wa miaka 23, anataka kikao cha ana kwa ana na kocha wa Newcastle, Alan Pardew kabla hajaamua kuondoka Ajax kujiunga na The Magpies.
Mshambuliaji wa Bolton, David Ngog, mwenye umri wa miaka 23, ametajwa kutakiwa na klabu ya Fulham ya Ligi Kuu.

WAGONGA NYUNDO KUMSAINI CARROLL

Mmiliki mshiriki wa West Ham, David Sullivan amesema klabu hiyo inajiandaa kuweka rehani fedha zake kwa kumsajili Andy Carroll, mwenye umri wa miaka 23, kutoka Liverpool.
ASHLEY COLE AMPA MEDALI SHABIKI BWANA MDOGO WA MANCHESTER CITY
Moyo wa kiuanamichezo unaweza kumuathiri beki wa kushoto wa Chelsea, Ashley Cole, kwa kitendo chake cha kumopa Medali yake ya Ngao ya Jamii, shabiki mtoto wa Manchester City.