Tetesi za Jumanne magazeti Ulaya
MAN UNITED WAFIKA BEI YA VAN PERSIE ARSENAL, FERGUSON AZUNGUMZA NA WENGER MWENYEWE KUMUHAKIKISHIA
KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amezungumza moja kwa moja na kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kujaribu kumuhakikishia yuko tayari kutoa pauni Milioni 20 kwa ajili ya mshambuliaji wa Kiholanzi, Robin van Persie, mwenye umri wa miaka 29.
Liverpool itatazamia kumbadili beki wake wa kati Daniel Agger kwa kumsajili beki wa Swansea, Ashley Williams, mwenye umri wa miaka 27, kama watamuuza Mdenmark huyo Manchester City.
Inter Milan imeungana na Chelsea na Liverpool katika mkakati wa kumsajili winga wa Arsenal, Theo Walcott. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 anamaliza mkataba wake msimu ujao.
Kiungo wa Real Madrid, Nuri Sahin ataamua mustakabali wake wiki hii baada ya Arsenal na Liverpool kujitokeza kumuomba kwa mkopo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23.
Aston Villa inaweza kumuuza beki Stephen Warnock, baada ya kocha Paul Lambert kuamua kumtazama kwa kina katika mechi ya kirafiki dhidi ya Werder Bremen. Hata hivyo, klabu hiyo bado haijapokea ofa yoyote kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30.
WELBECK APEWA MKATABA MPYA MREFU
Mshambuliaji wa Manchester United, Danny Welbeck, mwenye umri wa miaka 21, amekubali mkataba mpya wa miaka mitano, ambao sasa atakuwa analipwa pauni 75,000 kwa wiki.
Beki wa Liverpool, Martin Skrtel, mwenye umri wa miaka 27, atasaini mkataba mpya wa miaka minne wiki hii kubaki Anfield.
Mshambuliaji wa Tottenham, Jermain Defoe, mwenye umri wa miaka 29, hataki kuingia kwenye mwaka mwingine wa mateso ya kusugua benchi.
Kocha wa Spurs, Andre Villas-Boas hana uhakika wa kumpanga Sandro, mwenye umri wa miaka 23, katika mwechi ya ufunguzi ya LIgi Kuu England dhidi ya Newcastle Jumamosi, kwa sababu hajamuona kiungo huyo kwa sababu alikuwa na timu yake ya taifa, Brazil kwenye Michezo ya Olimpiki Jijini London.
Maumivu ya nyonga yanaweza kumfanya Marouane Fellaini, mwenye umri wa miaka 24, aikose mechi ya Everton na Manchester United Jumatatu ijayo.
No comments:
Post a Comment