Tuesday, November 6, 2012

WAZEE WA POWER WINDOW WAMLIZA MTANGAZAJI WA CLOUDS FM.

Siku chache  baada  ya msanii nyota wa muziki wa  kizazi  kipya  nchini Ommy Dimpoz kuibiwa  vifaa kutoka gari yake, mtangazaji mahiri wa  kipindi cha  'Kwa Raha Zetu' kinachorushwa na Clouds Fm ya jijini Gea Habib naye amekutana na dhahma  hiyo baada ya wakora  kuiba  vifaa kutoga ndinga  yake ya kisasa aina ya GX110.
 Gea amesema kuwa aliibiwa vitu hivyo mwishoni mwa wiki iliyopita maeneo ya Kigogo na siku moja  iliyopita alipigiwa simu na watu wasiojulikna  wakimtaka kutoa  kiasi cha shilingi milioni moja na nusu ili aweze  kuvipata tena  vifaa  hivyo.
 "Nimepigiwa simu 'leo' huyo mtu kaniambia  vifaa  vyangu vyote vipo  isipokuwa  natakiwa  nitoe shilingi Milioni1.5 kuvipata, hawa  watu hawana hata aibu  na inaelekea ni watu ambao  wanatufahamu na wanajua  kila mtangazaji  anamiliki gari gani" alisema Gea.
 
 
 PICHA  TOFAUTI ZA GARI YA GEA  HABIB  BAADA YA KUIBIWA  VIFAA MBALIMBAL

No comments: