Jacqline ameandika kwenye blog yake na namkariri akisema
“kiukweli mimi kama Jacquline Wolper sina ubaya na mtu yeyote, ila
nmeshangaa kuona watu nisiyo wajua kuja usiku wa manane na kunichomea
gari yangu. Kiukweli siwezi kumuhisi mtu ila najua ni lazima atakua mtu
asiependa maendeleo yangu ni ni mtu mbaya sana kwangu. Na inawezekana
kabisa alipanga kunia lakni kwa bahati nzuri siku hiyo sikua nyumbani
nilikua nimesafiri. Tukio lilitokea usiku wa tarehe 23/10/2012 ambapo
mtu alitumia matambara yaliyo na mafuta ya taa au Petrol akiwa kwa nje
ya ukuta wa nyumba yangu akiwa anarusha kwa ndani. Nimepeleka taarifa
kituo cha Polisi kawe kwa kutaka msaada wa kiupelezi na nitakua nawapa
taarifa za kila kinachoendelea. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwani niko
salama”
No comments:
Post a Comment