
David Villa.
Daktari wa klabu ya
Barcelona, Ramon Cugat amesema kuwa mshambuliaji nyota wa timu hiyo
David Villa amepona mguu wake ambao ulivunjika. Mshambuliaji huyo wa
kimataifa kutoka Hispania amkuwa nje ya uwanja toka alipofanyiwa
upasuaji Desemba mwaka jana lakini mchezaji huyo bado anahitaji muda
zaidi ili
aweze kupona kwa asilimia mia moja. Barcelona walipata tabu
bila ya kuwepo kwa Villa mwenye umri wa miaka 30 msimu uliopita ingawa
timu ya taifa ya Hispania yenyewe ilifanikiwa kutetea taji lake la Ulaya
bila ya kuwepo mshambuliaji huyo anayeoongoza kwa mabao katika kikosi
hicho. Daktari huyo pia amesema kuwa kiungo Thiago Alcantara na Isaac
Cuenca bado hawajapona majeraha yanayowasumbua. Barcelona inatarajiwa
kucheza mchezo wake wa kwanza Agosti 19 dhidi ya Real Sociedad katika
Ligi Kuu nchini Hispania inayojulikana zaidi kama La Liga.
No comments:
Post a Comment