Wednesday, August 15, 2012

RIBERY, BENZEMA WAKABILIWA NA TUHUMA ZA UKAHABA.

Wachezaji nyota wa kimataifa wa Ufaransa, Franck Ribery na Karim Benzema wanatarajiwa kuitwa mbele ya jaji kujitetea juu ya tuhuma za kutembea na msichana kahaba mwenye umri chini ya miaka 18. Wachezaji hao ambao wamo katika kikosi cha nchi hiyo ambacho kitacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Uruguay baadae leo, walikuwa wanachunguzwa kuhusiana na tuhuma hizo miaka miwili iliyopita. Wote wawili
walikana mashitaka hayo na msichana anayehusika ambaye anaitwa Zahia Dehar amesema kuwa hakuna mchezaji yoyote kati ya hao aliyekuwa akijua kuwa ana miaka 16 katika kipindi hicho. Hakina anayesimamia kesi hiyo amesema kuwa wachezaji hao wanatakiwa kutoa ushahidi wao lakini hakuna tarehe iliyopangwa kwa ajili ya kesi hiyo. Chini ya Sheria za ufaransa kuchukua kahaba ambaye yuko chini ya umri wa miaka 18 inaweza pelekea ukapewa adhabu ya ya miaka mitatu jela na faini ya dola 55,000, hatahivyo mtuhumiwa anakiwa awe ametenda kosa hilo huku akijua kuwa aliyekuwa naye yuko chini ya miaka 18.

No comments: