Friday, August 10, 2012

PICHA 8 ZA TAIFA STARS WAKIFANYA WAKIFANYA MAANDALIZI YA KUWAVAA BOTSWANA.

Juma Kaseja mazoezini.
 Timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo imeanza maandalizi ya mchezo wake wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Botswana utakaochezwa Jumatano ijayo mjini Gaborone.
Stars ikiwemo Uwanja wa Karume jioni ya leo, na kuwakuta wachezaji wa timu hiyo wakijifua chini ya walimu wao, Mdenmark Kim Poulsen na wasaidizi wake Sylvester Marsh na Juma Pondamali.
Wachezaji waliokuwapo mazoezini ni makipa Deogratias Munishi (Azam), nahodha Juma Kaseja (Simba) na Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni nahodha msaidizi Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga) na Shomari Kapombe (Simba).

Viungo ni Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Moshi (Simba), Mrisho Ngassa (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Ramadhan Chombo (Azam), Ramadhan Singano (Simba), Salum Abubakar (Azam) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Said Bahanuzi (Yanga), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC).
Stars inayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, itaondoka Dar es Salaam Jumanne. 


John Bocco kulia, nyuma yake ni kocha Poulsen.

Bocco kulia na Poulsen.

Bahanuzi na Boban kulia.

Ngassa na Bahanuzi kulia.

Bocco na Boban kujia.

Ngassa na Nyoni.

Kocha wa makipa Juma Pondamali kulia, akiwaongoza makipa Kaseja, Dida na Mwadini.

No comments: