Thursday, August 16, 2012

HUYU NDIO MTANGAZAJI TV MAARUFU SHABIKI WA ARSENAL ALITISHIA KUJIUA ENDAPO VAN PERSIE ANGEONDOKA ARSENAL.

Mtangazaji maarufu wa kituo cha CNN raia wa Uingereza Piers Morgan ambaye anatambulika kwa mapenzi yake aliyonayo juu ya klabu ya Arsenal FC - Piers Morgan jana alitoa mpya katika mtandao wa Twitter.
Huku kukiwa kumebakiwa na masaa kadhaa kabla ya Arsenal kuthibitisha kwamba wamekubalina bei ya ada ya uhamisho wa Robin van Persie kwenda Manchester United, Piers Morgan alikuwa akitoa kauli za kuomba nahodha wao asiondoke klabuni kwao, na hata kama ikiwa anaondoka basi asiuzwe kwa klabu ambayo anadai ni wapizani wao nchini Uingereza.

Baada ya mfululizo wa tweets za namna hiyo baadae kama alifikiria nini kitatokea baada ya muda mchache akaandika tweet iliyokuwa na ujumbe wa moja kwa moja kwenda Van Persie ukisema "Sio kama nakupa presha Van Persie - lakini ikiwa utaondoka #Arsenal then nitaenda kujirusha mwenyewe kwenye daraja la Santi Monica."

No comments: