Tetesi za Alhamisi magazeti Ulaya


CHICHARITO AMKIMBIA VAN PERSIE MAN UNITED
Huku Manchester United ikijiandaa kumsajili Nahodha wa Arsenal, Robin van Persie, mshambuliaji wa Old Trafford, Javier Hernandez 'Chicharito', mwenye umri wa miaka 24, anaweza kuondoka.
Kocha wa Croatia, Igor Stimac ameanzisha mashambulizi na Daniel Levy, akimtuhumu Mwenyekiti huyo, Tottenham kukiuka ahadi zao na Luka Modric, mwenye umri wa miaka 26, kuhusu kuhamishiwa Real Madrid.
Sunderland imeanza mazungumzo na mchezaji huru Louis Saha, mwenye umri wa miaka 34, huku majadiliano mengine na Wolves yakiendelea kuhusu Steven Fletcher.
Jermain Defoe scored for England in their 2-1 win over Italy
Jermain Defoe alifunga bao katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Italia
QPR, Aston Villa na Sunderland zote bado zina nia ya kumsajili mshambuliaji wa Tottenham na England, Jermain Defoe, mwenye umri wa miaka 29.
Everton inajiandaa kumsajili kiungo wa Liverpool, Charlie Adam, mwenye umri wa miaka 26, ambaye ataruhusiwa kuondoka Anfield kwa dau la pauni Milioni 5.

WAMILIKI WA ZAMANI WAWATESA WAMILIKI WAPYA LIVERPOOL

Mmiliki wa Liverpool, John W Henry amesema kwamba Liverpool bado inaumia na makovu ya wamiliki wa zamani wa klabu hiyo waliochemsha.
Kiungo wa zamani wa Arsenal, Ray Parlour anaamini kuuzwa kwa Robin van Persie kunaonyesha Arsenal haiwezi tena kushindana na klabu kubwa.

AC MILAN YASAJILI BINTI WA MIAKA 10


AC Milan imemsajili binti wa umri wa miaka 10 kutoka East Dunbartonshire, baada ya kuwavutia wasaka vipaji wa klabu hiyo huko La Manga.