Tuesday, August 21, 2012

ADEBAYOR AKUBALI MSHAHARA KIDUCHU AACHANE NA MAN CITY, ATUE JUMLA SPURS.

 Emmanuel Adebayor anatumai kukamilisha uhamisho wa pauni Milioni 5, kutua moja kwa moja Spurs wiki hii.
Makubaliano yalikwishafikiwa baina ya Manchester City na klabu hiyo ya White Hart Lane, zaidi ya wiki sita
zilizopita, lakini yalikwama kutokana na Adebayor juu ya maslahi yake binafsi.
Lakini Adebayor sasa ameonyesha yuko tayari kupokea mshahara wa chini, kutoka ule aliokuwa akipewa awali katika mkataba wa City.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Togo, amebakiza miaka miwili kwenye mkataba wake wa mshahara wa pauni 170,000 kwa wiki, aliosaini akijiunga na City mwaka 2009 kutoka Asrenal.
Mabingwa City watapata hasara kwa mchezaji huyo waliyemnunua pauni Milioni 25 kutoka Arsenal. Kocha Mtaliano, Roberto Mancini alisema hivi karibuni: “Samahani kwa Adebayor, kwa sababu ni mchezaji mzuri. Hakuna nafasi kwa yeye kucheza kwetu, hivyo kwa sababu hiyo, ni muhimu tumepata suluhisho.”

No comments: