Tuesday, August 21, 2012

BEKI LA MALI LAMFUNGISHA VIRAGO MUDDE SIMBA SC.

Mussa Mudde kushoto akichezea Simba.
Ujio wa beki kutoka Mali, Komalmbil Keita unahatarisha maisha ya kiungo wa Simba, Mussa Mudde wa Uganda, ambaye ni majeruhi.
Hivi karibuni, Simba iliwavuta wachezaji wa kigeni, Mghana Danniel Akuffo na beki wa Kenya, Pascal Ochieng na kufanya iwe na idadi kubwa ya wachezaji wa kigeni.
Kutokana na hali hiyo, Simba sasa inatakiwa kupunguza mchezaji mmoja wa kigeni iwapo Keita atafuzu majaribio Msimbazi.

ADEBAYOR AKUBALI MSHAHARA KIDUCHU AACHANE NA MAN CITY, ATUE JUMLA SPURS.

 Emmanuel Adebayor anatumai kukamilisha uhamisho wa pauni Milioni 5, kutua moja kwa moja Spurs wiki hii.
Makubaliano yalikwishafikiwa baina ya Manchester City na klabu hiyo ya White Hart Lane, zaidi ya wiki sita

DAVID SILVA KUONDOKA MAN CITY, LIVERPOOL HAIMTAKI ANDY CARROLL.


Gossip logo
20 August 2012Last updated at 22:49 GMT

Tetesi za J'nne magazeti ya Ulaya


DAVID SILVA KUONDOKA MAN CITY, LIVERPOOL HAIMTAKI ANDY CARROLL

Manchester City inaweza kumpoteza kiungo wake nyota, David Silva, aliyezaliwa miaka 26 iliyopita, baada ya mazungumzo ya kuongeza mkataba naye kuvunjika.
Andy Carroll
Andy Carroll anatakiwa na West Ham na Newcastle 
Liverpool itamuambia Andy Carroll, mwenye umri wa miaka 23, aamue mustakabali wake hadi mwishoni mwa wiki hii, huku Wekundu hao wakifikiria kumuuza Tottenham, iliyoonyesha nia ya kumsajili.
Mchezaji anayetakiwa na Manchester City, Daniele De Rossi, mwenye umri wa miaka 29, anajianda kukataa ofa ya klabu hiyo ya Ligi Kuu England, abaki Roma.
West Ham inajipanga kujaribu bahati yake kwa kiungo Matt Jarvis, mwenye umri wa miaka 26, huku wakiwa karibu kumnasa winga mwenye umri wa miaka 25 wa Rennes, Razak Boukari.
Queens Park Rangers inataka kumsajili beki wa Tottenham, Michael Dawson, mwenye umri wa miaka 28.
Habari kamili: The Times  (subscription required)
Tottenham haina nia ya kumsajili m shambuliaji wa Arsena, Marouane Chamakh mwenye umri wa miaka 28.
Tottenham inataka kumfuata kiungo wa Roma, Miralem Pjanic, mwenye umri wa miaka 22, kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
Sunderland haitapigwa bao katika mshahara au ada ya uhamisho na klabu nyingine zinazomuwania pia, kiungo wa Manchester City, Adam Johnson, aliyezaliwa miaka 25 iliyopita.
Roberto Martinez
Kocha wa Wigan, Roberto Martinez alikuwa anatakiwa na Liverpool
Kipa wa Blackburn, Mark Bunn, mwenye umri wa miaka 27, anatakiwa na klabu ya Norwich City.
Wolves imewaambia wachezaji wanaotaka kuondoka, Steven Fletcher na Matt Jarvis kuzingatia mikataba yao na kubaki Molineux.

MARTINEZ AFICHUA KUHUSU LIVERPOOL

Roberto Martinez amesema alikataa kazi ya kuikochi Liverpool.
Eden Hazard, aliyezaliwa miaka 21 iliyopita, anaamini hatasumbuliwa na kupigwa 'ngwala za nguvu' na mabeki wa Ligi Kuu, baada ya kuuanza vizuri msimu akiwa na Chelsea.
Habari kamili: The Times  (subscription required)

BALOTELLI SASA APOKONYA LENZI ZA WAPIGA PICHA

Mario Balotelli amegundua njia mpya ya kuwazuia wapiga picha kumpiga picha, anawachukulia lenzi zao.

HII NDIO NGOMA MPYA YA PAH ONE - ASAMBEE.

 

Saturday, August 18, 2012

UJUMBE WA KIPANYA JANA.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgiGEZJDyx2JhyphenhyphenXIOeeQKMOfkW_cLnWzGAOGLsYD7k4a9isikovyrisuydmm53iGxz_hwmLKZIbJiwj4rUcjIsKUifw5DPQqgFI6lqzE-KTl2EoyuI7GMXxfQMouK0dKF6mjDjESZE5oAo/s640/SAM_4599.JPG

MANCINI AREJESHA KOMBE OLD TRAFFORD MAPEMAAAAA.

NANI KAISAHAU HII? 
 Kocha wa Manchester City, Roberto Mancini amesema jirani zake, United wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England - kwa sababu wana washambuliaji wawili wakali mno.
Mashetani Wekundu wamemnunua Robin van Persie kutoka Arsenal kwa pauni Milioni 24 na watamtumia kwa pamoja na Wayne Rooney pale mbele

LIGI KUU ENGLAND YAANZA LEO; PREVIEW WIGAN NA CHELSEA HILI HAPA.

Eden Hazard
Eden Hazard.

     VIKOSI VYA LEO
WIGAN

Al-HabsiRamis, Caldwell, Figueroa
Boyce, McCarthy, McArthur, Beausejour
Miyaichi, Di Santo, Maloney
   
CHELSEA

CechIvanovic, Terry, Cahill, Cole
Mikel, Lampard
Ramires, Mata, HazardTorres

WACHINA NOMA, WATENGENEZA HADI SAINI FEKI YA MARADONA.

Diego Maradona - Al Wasl
 Diego Maradona.
 Gwiji wa soka Argentina, Diego Maradona (pichani) ameingia kwenye zengwe lingine, la kufojiwa kwa saini yake na msaidizi wake wa zamani. Maradona anaelezwa kujiandaa kushitaki kampuni mbili za China, Sina na The 9 Limited, baada ya kutumia picha na jina lake kwenye soka yao 'Hot Blooded Soccer' bila ridhaa yake, . Ilidhaniwa saini ni ya mwenyewe kocha huyo wa zamani wa Argentina, lakini Maradona amesema hajawahi kusaini makubaliano hayo.  

LIVERPOOL YASAJILI KIFAA CHA MOROCCO.

Oussama Assaidi, sc Heerenveen
 Liverpool imekamilisha usajili wa winga wa kimataifa wa Morocco,Oussama Assaidi kutoka klabu ya Heerenveen kwa mujibu wa Goal.com.

LUIS NANI KUONDOKA MAN UNITED, OSCAR AWAPA MANENO WANAYOTAKA KUSIKIA CHELSEA..


Gossip logo
17 August 2012Last updated at 22:45 GMT

Tetesi za J'mosi magazeti ya Ulaya


LUIS NANI KUONDOKA MAN UNITED

Zenit St Petersburg sasa inamtaka winga wa Manchester United, Nani, mwenye umri wa miaka 25.
West Ham iko tayari kuzipiku Liverpool na Arsenal katika usajili wa mshambuliaji wa Fulham, Clint Dempsey, mwenye umri wa miaka 29.
Wakati huo huo, klabu hiyo ya Craven Cottage imekataa dau dogo la Manchester United kumtaka kiungo Moussa Dembele, 25.
Fulham midfielder Moussa Dembele
Moussa Dembele alijiunga na Fulham mwaka 2010
Beki wa Toulouse, Cheikh M'Bengue, mwenye umri wa miaka 24, amesema anatakiwa na Arsenal.
Stoke imeungana na Everton katika kuwania saini ya kiungo wa Liverpool, Charlie Adam, mwenye umri wa miaka 26.
Everton itamtoa kwa mkopo kiungo Ross Barkley, mwenye umri wa miaka 18, kwenda klabu ya Daraja la Kwanza, Sheffield Wednesday ambako wanaamini atapata uzoefu wa haraka wa kucheza katika kikosi cha kwanza.
Blackburn imeongeza ofa yake kwa ajili ya mshambuliaji wa Huddersfield, Jordan Rhodes, mwenye umri wa miaka 22.
Mshambuliaji Kevin Mirallas, mwenye umri wa miaka 24, atafanyiwa vipimo vya afya Everton mwishoni mwa wiki hii, kabla ya kukamilisha uhamisho wa pauni Milioni 5.3, akitokea Olympiacos.

OSCAR ASEMA HANA JAKAMOYO

Chelsea and Brazil midfielder Oscar
Oscar amewasili Chelsea akitokea Internacional
Mchezaji mpya wa Chelsea, Oscar amesema kwamba hasikii jakamoyo kabisa Stamford Bridge - kwa sababu tayari amefanikiwa kupata jezi namba 10 ya Brazil.
Sir Alex Ferguson amesema kwamba amekuwa mkali mno kwa wachezaji wake wa Manchester United wanaotumia Twitter, baada ya Rio Ferdinand kupigwa faini ya pauni 45,000 na FA.
Kiungo mstaafu wa Bolton, Fabrice Muamba atafanikiwa tu katika maisha yake kwa uamuzi wowote atakaochukua- kwa mujibu wa Nahodha, Kevin Davies.
Kipa wa Celtic, Fraser Forster amedhamiria kupambana kupata nafasi katika kikosi cha England kwa kufanya vitu adimu katika Ligi ya Mabingwa.

Thursday, August 16, 2012

ZAMARADI, RAY KIMENUKA.

Mtangazaji wa Kipindi cha ‘Take One’ cha Clouds Tv ya jijini Dar, Zamaradi Mketema na staa wa filamu za Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ kimenuka.
Chanzo kinasema kiini cha tifu lao ni kufuatia mtangazaji huyo kurusha kipindi akimuhoji mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ney wa Mitego akisema ‘ukitaka mwanamke malaya nenda Bongo Movie’. Baada ya kurusha kipindi hicho, inasemekana Ray alikereka na kuwataka wasanii wa Bongo Movie kutofanya kipindi na Zamaradi kwa madai aliwadhalilisha.

UJUMBE WA KIPANYA LEO.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiHQmutV4l-8E5vRRmU3J8kp_zPAy-Y2WjGXRaQCh_NnaqMbPlLVcUva2yHWrUie0JfMIb0UG730SaWFNJOATWPdhRs3eiYAeGHjdCvvkZ6z24m5Xm72eZsNIEwqrD_meVTK00HoWxrCiw/s1600/SAM_4531.JPG

HUYU NDIO MTANGAZAJI TV MAARUFU SHABIKI WA ARSENAL ALITISHIA KUJIUA ENDAPO VAN PERSIE ANGEONDOKA ARSENAL.

Mtangazaji maarufu wa kituo cha CNN raia wa Uingereza Piers Morgan ambaye anatambulika kwa mapenzi yake aliyonayo juu ya klabu ya Arsenal FC - Piers Morgan jana alitoa mpya katika mtandao wa Twitter.
Huku kukiwa kumebakiwa na masaa kadhaa kabla ya Arsenal kuthibitisha kwamba wamekubalina bei ya ada ya uhamisho wa Robin van Persie kwenda Manchester United, Piers Morgan alikuwa akitoa kauli za kuomba nahodha wao asiondoke klabuni kwao, na hata kama ikiwa anaondoka basi asiuzwe kwa klabu ambayo anadai ni wapizani wao nchini Uingereza.

HIZI NDIO HASIRA ZA MASHABIKI WA ARSENAL DHIDI YA VAN PERSIE.

Muda mchache baada ya vilabu vya Arsenal na Man United kuthibitisha kwamba vimekubalina ada ya uhamisho wa mchezaji RobinVan Persie kujiunga na mashetani wekundu - baadhi ya mashabiki wa Arsenal wamekuwa wakipost picha mitandaoni kuonyesha namna walivyopokea taarifa za nahodha wao kwenda Old Traford. Wapenzi wa Arsenal vipi? KAMA YOYOTE AMBAYE ANATAKA KUONYESHA HASIRA ZAKE KAMA HAWA ATUME PICHA AU MAONI KWENYE EMAIL HII - johnson.malimali@gmail.com 

ROBIN VAN PERSIE NA CESC FABREGAS, WALIVYOFANYA TAREHE 15 AUGUST KUWA MBAYA KATIKA HISTORIA YA ARSENAL.

Tarehe 15 ya August itaendelea kuwa tarehe ya maumivu kwa washabiki wa Arsenal milele.
Kwanini?
Msimu uliopita mnamo tarehe 15, mwezi kama huu yaani August, Arsenal walimuuza nahodha wao na kiungo wa kutegemewa Cesc Fabregas waliomsajili na kukaa nae kwa takribani miaka 8.

CHICHARITO AMKIMBIA VAN PERSIE MAN UNITED.



Gossip logo
15 August 2012Last updated at 22:49 GMT

Tetesi za Alhamisi magazeti Ulaya


CHICHARITO AMKIMBIA VAN PERSIE MAN UNITED
Huku Manchester United ikijiandaa kumsajili Nahodha wa Arsenal, Robin van Persie, mshambuliaji wa Old Trafford, Javier Hernandez 'Chicharito', mwenye umri wa miaka 24, anaweza kuondoka.
Kocha wa Croatia, Igor Stimac ameanzisha mashambulizi na Daniel Levy, akimtuhumu Mwenyekiti huyo, Tottenham kukiuka ahadi zao na Luka Modric, mwenye umri wa miaka 26, kuhusu kuhamishiwa Real Madrid.
Sunderland imeanza mazungumzo na mchezaji huru Louis Saha, mwenye umri wa miaka 34, huku majadiliano mengine na Wolves yakiendelea kuhusu Steven Fletcher.
Jermain Defoe scored for England in their 2-1 win over Italy
Jermain Defoe alifunga bao katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Italia
QPR, Aston Villa na Sunderland zote bado zina nia ya kumsajili mshambuliaji wa Tottenham na England, Jermain Defoe, mwenye umri wa miaka 29.
Everton inajiandaa kumsajili kiungo wa Liverpool, Charlie Adam, mwenye umri wa miaka 26, ambaye ataruhusiwa kuondoka Anfield kwa dau la pauni Milioni 5.

WAMILIKI WA ZAMANI WAWATESA WAMILIKI WAPYA LIVERPOOL

Mmiliki wa Liverpool, John W Henry amesema kwamba Liverpool bado inaumia na makovu ya wamiliki wa zamani wa klabu hiyo waliochemsha.
Kiungo wa zamani wa Arsenal, Ray Parlour anaamini kuuzwa kwa Robin van Persie kunaonyesha Arsenal haiwezi tena kushindana na klabu kubwa.

AC MILAN YASAJILI BINTI WA MIAKA 10


AC Milan imemsajili binti wa umri wa miaka 10 kutoka East Dunbartonshire, baada ya kuwavutia wasaka vipaji wa klabu hiyo huko La Manga.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS AUG 16 2012.

Wednesday, August 15, 2012

WHAT! KANYE WEST CALLS KIM K 'Bitch' WHILE 50 CENT LABELS HER 'Trash'!

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjOZFraLVStYBwUftybaorXUfhZrC3drFQpCPFiJE5c_aVDdZ5GfNON3GyA0Jm414W08EbL1Q5T6nvPwx8R4q5IT2Ja2lNCJnBzgrDb3ih24bd49uJq52cwZtFmWi1poLhEF_znBLRIbOdq/s1600/Kim+K_50+Cent.jpg
Does a man always have to trash his rival's girlfriend or wife to get to him? Ok, we all know Kanye called his girlfriend, Kim K, 'perfect bitch' but does that give 50cent the audacity to term her Trash? *Just asking oh*. Really, the Kadashians are not my favourite TV personalities but then, they're doing their thing and gaining popularity not to talk of making some good money from it.

UJUMBE WA KIPANYA LEO.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjMy4xSTPqJs34oxvuAwynAqd7kfTHyTIY_UNxyRyDk-W4TRrRCKMqke2kLS7XhdKOeqClMwAqWdAQRB7-SZyjZ92q3wzdDoFqj1Zdi1XWkw9k4eQsCDPB023cfK2gUMyungD1vVtHavoTu/s1600/SAM_4524.JPG

HII NDIO NGOMA MPYA YA PROFFESOR JAY FT DULLY SYKES - HELLOW.





RIBERY, BENZEMA WAKABILIWA NA TUHUMA ZA UKAHABA.

Wachezaji nyota wa kimataifa wa Ufaransa, Franck Ribery na Karim Benzema wanatarajiwa kuitwa mbele ya jaji kujitetea juu ya tuhuma za kutembea na msichana kahaba mwenye umri chini ya miaka 18. Wachezaji hao ambao wamo katika kikosi cha nchi hiyo ambacho kitacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Uruguay baadae leo, walikuwa wanachunguzwa kuhusiana na tuhuma hizo miaka miwili iliyopita. Wote wawili

KANYE WEST, RICK ROSS, DJ KHALED HAWA HAPA KWENYE NEW VIDEO! KIM K PIA.


MAGAZETI YA LEO JUMATANO AUG 15 2012.

STARS WAKIWAKUSANYIA UPEPO PUNDA MILIA GABORONE.

Wachezaji wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars wakiwa mazoezini katika Viwanja vya benki ya Botswana kujiandaa na mechi dhidi ya The Zebras ya Botswana ambayo inatarajiwa kupigwa leo jioni nje kidogo ya Mji wa Gaborone.

MAN UNITED WAIPIGA BAO NJE YA UWANJA MANCHESTER CITY, VAN PERSIE ATUA OLD TRAFFORD KWA PAUNI MILIONI 22 AU 25.


Gossip logo
14 August 2012Last updated at 22:41 GMT

Tetesi za J'tano magazeti ya Ulaya


MAN UNITED WAIPIGA BAO NJE YA UWANJA MANCHESTER CITY

Kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amewapiku jirani zake, Man City katika kuwania saini ya mshambuliaji wa Chile, Angelo Henriquez, mwenye umri wa miaka 18.
Hulk
Mshambuliaji Mbrazil, Hulk anaweza kutua England
Arsenal inajipanga kumruhusu Robin van Persie, mwenye umri wa miaka 29, kujiunga na Manchester United kwa dau la pauni Milioni 22.
Lakini taarida nyingine zinasema kwamba Arsenal wanataka angalau pauni Milioni 25 kutoka Manchester United kwa ajili ya Van Persie.
Chelsea na Manchester City ziko mkao wa kula, kufuatia mshambuliaji wa Porto, Hulk, mwenye umri wa miaka 26, kusema yuko tayari kuihama klabu hiyo ya Ureno.
Manchester City inafikiria kuongeza vipaji zaidi vya Kiingereza kwenye kikosi chake, baada ya kumsajili Jack Rodwell na Scott Sinclair, Jack Butland na Nathan Redmond wakiwa wanatajwa kufuatiliwa na mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England.
Tottenham na Arsenal zitatakiwa kulipa pauni Milioni 28 kumsajili nyota wa kimataifa wa Hispania, Fernando Llorente, kwa mujibu wa rais wa klabu yake, Athletic Bilbao, Josu Urrutia.
Liverpool imemtuma Mkurugenzi wake Mtendaji, Ian Ayre kwenda Hispania kushughulikia usajili wa winga wa Barcelona, Cristian Tello, mwenye umri wa miaka 21, na kiungo wa Real Madrid, Nuri Sahin, mwenye umri wa miaka 23.
Andy Carroll
Mshambuliaji wa Liverpool, Carroll anaweza kutua West Ham
Everton inataka kutumia sehemu ya fedha ilizopata kutokana na mauzo ya Jack Rodwell, mwenye umri wa miaka 21, kwenda Manchester City kwa kumsajili Kevin Mirallas, mwenye umri wa miaka 24, kutoka Olympiacos kwa dau la pauni Milioni 6.
Habari kamili: The Times  (subscription required)
Vurnon Anita, mwenye umri wa miaka 23, anataka kikao cha ana kwa ana na kocha wa Newcastle, Alan Pardew kabla hajaamua kuondoka Ajax kujiunga na The Magpies.
Mshambuliaji wa Bolton, David Ngog, mwenye umri wa miaka 23, ametajwa kutakiwa na klabu ya Fulham ya Ligi Kuu.

WAGONGA NYUNDO KUMSAINI CARROLL

Mmiliki mshiriki wa West Ham, David Sullivan amesema klabu hiyo inajiandaa kuweka rehani fedha zake kwa kumsajili Andy Carroll, mwenye umri wa miaka 23, kutoka Liverpool.
ASHLEY COLE AMPA MEDALI SHABIKI BWANA MDOGO WA MANCHESTER CITY
Moyo wa kiuanamichezo unaweza kumuathiri beki wa kushoto wa Chelsea, Ashley Cole, kwa kitendo chake cha kumopa Medali yake ya Ngao ya Jamii, shabiki mtoto wa Manchester City.

Tuesday, August 14, 2012

MAN UNITED WAFIKA BEI YA VAN PERSIE ARSENAL, FERGUSON AZUNGUMZA NA WENGER MWENYEWE KUMUHAKIKISHIA.



Gossip logo
13 August 2012Last updated at 22:47 GMT

Tetesi za Jumanne magazeti Ulaya


MAN UNITED WAFIKA BEI YA VAN PERSIE ARSENAL, FERGUSON AZUNGUMZA NA WENGER MWENYEWE KUMUHAKIKISHIA 

KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amezungumza moja kwa moja na kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kujaribu kumuhakikishia yuko tayari kutoa pauni Milioni 20 kwa ajili ya mshambuliaji wa Kiholanzi, Robin van Persie, mwenye umri wa miaka 29.
Liverpool itatazamia kumbadili beki wake wa kati Daniel Agger kwa kumsajili beki wa Swansea, Ashley Williams, mwenye umri wa miaka 27, kama watamuuza Mdenmark huyo Manchester City.
Manchester United hope to sign Robin van Persie before the Premier League begins this weekend
Manchester United ina matumaini ya kumnasa Robin van Persie kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu
Inter Milan imeungana na Chelsea na Liverpool katika mkakati wa kumsajili winga wa Arsenal, Theo Walcott. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 anamaliza mkataba wake msimu ujao.
Kiungo wa Real Madrid, Nuri Sahin ataamua mustakabali wake wiki hii baada ya Arsenal na Liverpool kujitokeza kumuomba kwa mkopo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23.
Aston Villa inaweza kumuuza beki Stephen Warnock, baada ya kocha Paul Lambert kuamua kumtazama kwa kina katika mechi ya kirafiki dhidi ya Werder Bremen. Hata hivyo, klabu hiyo bado haijapokea ofa yoyote kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30.

WELBECK APEWA MKATABA MPYA MREFU

Mshambuliaji wa Manchester United, Danny Welbeck, mwenye umri wa miaka 21, amekubali mkataba mpya wa miaka mitano, ambao sasa atakuwa analipwa pauni 75,000 kwa wiki.
Beki wa Liverpool, Martin Skrtel, mwenye umri wa miaka 27, atasaini mkataba mpya wa miaka minne wiki hii kubaki Anfield.
Marouane Fellaini has made 137 appearances for Everton since he joined the club in 2008
Marouane Fellaini amecheza mechi 137 Everton tangu ajiunge nayo mwaka 2008
Mshambuliaji wa Tottenham, Jermain Defoe, mwenye umri wa miaka 29, hataki kuingia kwenye mwaka mwingine wa mateso ya kusugua benchi.
Kocha wa Spurs, Andre Villas-Boas hana uhakika wa kumpanga Sandro, mwenye umri wa miaka 23, katika mwechi ya ufunguzi ya LIgi Kuu England dhidi ya Newcastle Jumamosi, kwa sababu hajamuona kiungo huyo kwa sababu alikuwa na timu yake ya taifa, Brazil kwenye Michezo ya Olimpiki Jijini London.
Maumivu ya nyonga yanaweza kumfanya Marouane Fellaini, mwenye umri wa miaka 24, aikose mechi ya Everton na Manchester United Jumatatu ijayo.